Tuesday, August 31, 2010

VYAMA VINNE HAVIJAZINDUA KAMPENI MPAKA SASA

Ndugu wadau, nitaendelea kuwaletea matukio mbalimbali ya uzinduzi rasmi wa kampeni ya vya vingine ambavyo hajazindua mpaka sasa. Vyama ambavyo havijazindua ni TLP, UPDP, NCCR-Mageuzi na APPT- Maendeleo.

Mgombea urais wa TLP ni Mutamwega Mugahywa, UPDP ni Fahmi Dovutwa, NCCR-Mageuzi ni Hashim Rungwe na mgombea urais wa APPT- Maendeleo ni Peter Mziray, lakini Mziray anadai chama chake kimezindua kampeni ingawa hakijaonekana kikifanya hivyo. Baadhi ya wagombea ubunge na udiwani wa vyama hivyo, wameanza kampeni.

Kumekuwepo malalamiko kwa waandishi wa habari kutoandika habari za vyama vingine vidogo. Baadhi ya watu wanadai waandishi wanaandika habari za vyama vitatu tu yaani za Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chadema na za Chama cha Wananchi CUF. Mgombea urais wa APPT- Maendeleo, Mziray anasema waandishi wanaandika habari za vyama ambavyo vinaweza kulipa gharama za waandishi hao. Kwa upande wangu naahidi kufuatilia habari za vyama vingine.

No comments:

Post a Comment