Wednesday, August 4, 2010

WANAFUNZI 80 WANUSURIKA KUTEKETEA KWA MOTO

WANAFUNZI 80 waliokuwa wamelala katika bweni la Nyerere Shule ya Sekondari Rugambwa Manispaa ya Bukoba wamenusurika kufariki dunia baada ya bweni hilo kuteketea kwa moto usiku wa kuamkia jana. Tukio hilo, lilitokea saa 2:30 usiku wakati wanafunzi hao wakiwa wanasoma madarasani.Katika tukio hilo, vifaa vyote vya wanafunzi viliteteketea kwa moto.

Mwandishi wa Mwananchi ambaye alikuwa eneo la tukio alishuhudia zaidi ya wanafunzi 15 wakizimia na kupoteza fahamu na baadaye kukimbizwa katika hospitali ya mkoa Kagera kwa matibabu zaidi. Mazingira ya shule hiyo yalitawaliwa na vilio vya wananchi na wanafunzi katika giza nene na kamanda wa polisi wa Mkoa wa Kagera Henry Salewi alikuwa miongoni mwa viongozi walioshiriki kuimarisha usalama katika eneo hilo.

Mkuu wa sekondari hiyo ya wasichana Asha Mbanga alipoulizwa kwa njia ya simu alisema hana taarifa kuhusu tukio hilo kwani alikuwa safarini kutoka jijini Mwanza.

No comments:

Post a Comment