Tuesday, August 3, 2010

Utata wa Malecela na Lusinde watatuliwa


Hatimaye CCM wilayani Chamwino jana ilimaliza utata kwenye matokeo ya kura za maoni katika jimbo la Mtera ilipotangaza kuwa mwanasiasa mkongwe, John Malecela ameangushwa baada ya habari kusambaa kwa kasi kubwa kuwa Livinstone Lusinde hakuwa ameshinda.
Habari za ushindi wa Lusinde zilifunikwa na taarifa iliyosambaa kwa kasi jana kuwa mshindi wa kura za maoni kwenye jimbo hilo bado hajatangazwa rasmi na kwamba Malecela ndiye aliyekuwa akiongoza kwa kupata kura 5,652 dhidi ya 5,407 za Lusinde licha ya katibu wa CCM mkoani Dodoma kumtangaza kijana huyo kuwa ndiye mshindi.

Lakini jana, mkurugenzi wa uchaguzi wa CCM wilayani Chamwino ambaye pia ni katibu wa chama hicho kwenye wilaya hiyo, Edson Lihweuli aliitisha mkutano na waandishi wa habari na kumtangaza Lusinde kuwa mgombea wa ubunge kwa tiketi ya CCM kwenye uchaguzi mkuu ujao na hivyo kuthibitisha habari za kuanguka kwa Malecela, maarufu kama "tingatinga".

No comments:

Post a Comment