Thursday, August 12, 2010

NAPE HUYOOO AIBUKIA CHADEMA

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Nape Nauye jana alienda kwenye Mkutano Mkuu wa Chadema na bila kuchelewa wajumbe wa mkutano huo, walikuwa wakijaribu kumvika tagi yenye picha ya mgombea wa urais wa Chadema, Dk Willibrod Slaa. Awali ilielezwa kuwa Nape alikuwa anataka kujiunga na Chadema baada ya kuangushwa kwenye kura za maoni katika Jimbo la Ubungo jijini Dar es Salaam. Lakini jana Nape alisema ni mwanachama wa CCM na ataendelea kubaki CCM.

1 comment:

  1. Kaka unatupa mambo matamu ya news, lakini mbona habari za michezo huweki kwenye blog yako?

    ReplyDelete