Wednesday, August 4, 2010

Mtikila akwepa kifungo gerezani



MWENYEKITI wa DP, Mchungaji Christopher Mtikila amekubali kulipa deni alilokuwa anadaiwa na Paskazia Matete la Sh 9.8 milioni na kuachiwa huru.

Kama Mchungaji huyo ambaye ametangaza kugombea urais kupitia chama chama cha DP asingelipa deni hilo, angetumikia kifungu cha miezi sita gerezani na tayari juzi alianza kuonja joto la jiwe baada ya kulala mahabusu ya kituo cha polisi cha Msimbazi kwa kushindwa kulipa deni hilo.

Mtikila alihukumiwa kifungo cha miezi sita jela bila ya kuwepo mahakamani Julai 29 baada ya mahakama kukubali ombi la mdai huyo. Hakimu Joyce Minde alitoa hukumu hiyo kwa sharti kwamba ianze kutekelezwa baada ya Paskazia kulipa Sh600,000 kwa ajili ya gharama za kumhudumia mchungaji huyo wakati atakapokuwa kifungoni.Mwanamke huyo alilipa fedha hizo na ndipo hukumu hiyo ilipoanza kutekelezwa.

No comments:

Post a Comment