Saturday, August 21, 2010

KIKWETE AANGUKA WAKATI AKIHUTUBIA JANGWANI

Kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM), jana zimeingia dosari ikiwa ni siku ya kwanza katika uzinduzi wa kampeni zake katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam baada ya mgombea wake wa kiti cha urais, Jakaya Kikwete kuanguka jukwaani kutokana na kuishiwa nguvu.

Baada ya dakika 16 tangu alipoanza kuhutubia umati wa wanaCCM waliofurika katika viwanja hivyo, Kikwete alianza kuishiwa nguvu na kupepesuka, lakini walinzi wake walimdaka na kumpa msaada kwa kumdoa jukwaani.

Dakika 14 baadaye alirejea jukwaani huku akionyesha kuchoka na kuendelea na hotuba yake kwa dakika tano kabla ya kwenda kuketi meza kuu kwa dakika mbili na kuamua kuondoka katika viwanja hivyo.

Rais Kikwete aliwasili viwanja hivyo saa 7:45 mchana akifuatana na Mgombea Mwenza, Dk Mohamed Gharib Bilal na kupanda katika jukwaa kuu kuungana na viongozi kadhaa wa CCM na serikali akiwa na furaha.

1 comment: