Monday, August 30, 2010

WANAHABARI MMEPOTEA KATIKA TAALUMA YA HABARI

Ndugu mwana mapambano mwenzangu , mwanahabari na mwanaharakati mwenzangu , naomba kutumia fursa hii katika blog yako kuweka wazi au bayana juu ya hoja hii ya taaluma ya habari na vyombo vya habari kukiuka maadili ya kitaaluma .

"Kumeanza pia kujitokeza mtindo wa baadhi ya vyombo vya habari kutoripoti kabisa habari za baadhi ya vyama na wagombea. Baraza linapenda kuwakumbusha wenye vyombo vya habari na wahariri wao kuwa kibali cha kuendesha gazeti au kituo cha radio au runinga ni mali ya umma.

Leseni za vyombo vya habari hutolewa ili umma upewe taarifa; hili ndilo lengo la kwanza. Faida ya kifedha au mapenzi ya kisiasa sio sababu kuu inayofanya leseni ya chombo cha habari itolewe. Kwa hiyo wahariri wajitahidi kufanya kazi yao kwa uadilifu, na wamiliki wa vyombo wasiwashinikize kuacha kutangaza au kuandika habari muhimu katika kipindi hiki."
Hayo si maneno yangu ni manenno ya katibu mtendaji Baraza la Habari Tanzania , aliyosema kwa lengo la kutoa onyo kwa vyombo vya habari na waandishi wa habari .
Naweza kusema kama alijua kuwa wanataaluma ya habari pamoja na vyombo vya habari vimepotea katika taaluma hii , kama ilivyo ada waandishi na vyombo vyake wamekuwa vibaraka wa wagombea wa chama fulani katika kutangaza sera zake , kitendo cha televisheni ya Taifa (TBC) kukatisha hotuba ya mgombea kiti cha urais kupitia chama cha Chadema ni uvunjaji wa sheria na kukiuka haki ya msingi ya wananchi wa Tanzania katika upataji wa taarifa au habari .
Naaamini kabisa katika hali ya kawaida kituo kikubwa kama TBC na kinachoendeshwa kwa kodi za wananchi ni aibu kukatisha matangazo katikati ya hotuba kwa zaidi ya mara moja , ikumbukwe kuwa hii si mara ya kwanza dalili hizi au hali ilishajitokeza hata siku ile ya mgombea wa Chadema alipokuwa anaomba ufadhili .
Ni vyema tukakumbuka kuwa kutokuwepo kwa usawa katika vyombo vya habari ni dalili tosha za kusababisha uvunjaji wa amani ni vyema tukakumbuka juu ya mahuaji ya kimbali kule Rwanda na Burundi sekta ya habari ina nguvu kama sekta zingine za kitaifa , ifahamike kuwa watanzania kwa sasa wanajua haki zao zote na wanafaham nini kinaendele katika Taifa la Tanzania .

Ushauri wangu ni kuwa kwa vile TBC ni chombo cha kitaifa na kinawajibu wa kuwajibika kwa umma ni vyema Mtendaji Mkuu wa hicho chombo awaeleze umma juu ya swala hili kwani kuna hisia kali baina ya TBC na vyama vya upinzani katika kutokuwepo usawa wa kutoa taarifa na mbaya zaidi hii inaonekana wazi .




Mwandishi wa makala haya

ni Samwel Mtuwa

Anapatikana Minnesota ,

United State of America (USA)



No comments:

Post a Comment