Wednesday, September 1, 2010

MAMA ATOWEKA NYUMBANI MAZINGIRA YA KUTATANISHA


Catherine Cosmas (55), mkazi wa Ubungo Extenal jijini Dar es Salaam,jana ametoweka nyumbani katika mazingira ya kutatanisha juzi saa 3:00 usiku na kwenda kusikojulikana.

Mtoto wa mama huyo Grant Cosmas aliliambia Mwananchi kuwa mama yake aliondoka nyumbani muda huo na kwamba waliagana usiku kwa ajili ya kwenda kulala, lakini alitoka nje na kutokomea moja kwa moja.

Grant alisema kabla ya kuagana walikuwa wakitazama tamthilia na kwamba mama yake anasumbuliwa na ugonjwa wa kusahau baada ya kufanyiwa uperesheni ya kichwa kwa kuwa kichwa kilikuwa kikimuuma mara kwa mara .

Alifafanua kuwa mama yake alikuja Dar es salaam akitokea mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya matibabu tangu Machi mwaka huu na kwamba hawajawahi kupotea tangu afike hapa.

Grant alisema mama huyo alikuwa amevaa nguo ya rangi ya kahawia juu na sketi yenye maua meupe na alikuwa amejitanda khanga rangi nyekungu.

"Tangu amekuja hapa kwa matibabu hakuwahi kupotea, hii ni mara ya kwanza na tumemtafuta tangu jana hatukufanikiwa kumpata,"alisema Grant. Taarifa za kupotea kwa Catherine zimetolewa katika kituo cha polisi cha Urafiki na Muleba cha Mabibo jijini Dar es Salaam.
Alisema endapo mtu yoyote atamuona mama huyo, atoe taarifa katika kituo cha polisi kilichopo Urafiki, Muleba au wapige simu namba 0654 843262, 0717700531 na 0754593244.





No comments:

Post a Comment