Sunday, September 12, 2010

VODACOM MISS TANZANIA 2010

Mrembo wa Vodacom Miss Tanzania 2010, Genevieve Emmanuel akiwa kwenye gari aina ya Hyundai baada ya kushinda taji la urembo usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Gari hilo, alikabidhiwa na Mkurungezi Mtendaji wa Vodacom Dietlof Mare. (Picha zote na Venance Nestory)


Huyu ndio Miss Talenti wa mwaka 2010, Flora Martin



AY akitumbuiza katika shindano la Miss Tanzania.




Waandishi wa habari wakitazama shindano la Miss Tanzania


Baadhi ya washiriki wa Miss Tanzania wakiwa jukwaani katika ukumbi wa Mlimani City


Baadhi ya wageni wakifuatilia shindano la kumtafuta Miss Tanzania, lililofanyika usiku wa kuamikia leo katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Tuesday, September 7, 2010

WAREMBO 30 MISS TANZANIA HAWA HAPA

WAREMBO WAKIWA WAMEPOZI KATIKA SHINDANO LA KUMTAFUTA BALOZI WA REDDS

Washiriki 30 wakiwa wamepozi katika shindano la kumsaka Balozi wa Redds lililofanyika Kinyamwezi Pub, Mikocheni. Mshindi wa atatangazwa Jumamosi katika shindano la kumtafuta Miss Tanzania.

TENDWA AIONYA CCM


John Tendwa ambaye ni msajili wa Vyama Vya Siasa nchini amekishauri Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutotumia picha zilizopigwa katika maeneo ya Ikulu kwenye kampeni zake kwa kuwa zinawashawishi wananchi kukipigia kura na kwamba vyama vingine vya siasa haviwezi kuzipata picha hizo kutokana na kutoweza kupiga picha kwenye eneo la Ikulu.

Wednesday, September 1, 2010

MIKE TAYSON KUWASILI NCHINI DESEMBA

Mike Tayson

OBAMA AWAZUIA WATOTO WAKE KUTAZAMA TELEVISHENI

Rais wa Marekani Barack na mke wake, Michelle Obama wakiwa wameongozana na watoto wao, Malia Obama (12) na Sasha (9) ambaye baba yake amemshika begani. Wazazi hao, wamesema wanataka watoto wao waishi maisha ya kawaida na pia hawaruhusiwi kutazama televisheni katikati ya wiki na kompyuta wamekuwa wakitumia kwa ajili ya kufanya kazi za shule tu. Obama na Michelle hakuwakueleza ni kwanini wanawazuia watoto hao kuangalia televisheni muda mrefu.

APPT-MAENDELEO YAZINDUA KAMPENI BUGURUNI


CHAMA cha APPT-Maendeleo kimezindua kampeni yake na kusema kimeweka vipaumbele katika suala la afya, elimu, viwanda na ajira zaidi.
Katika mkutano wa ufunguzi wa kampeni, katika viwanja vya Buguruni Rozana, mgombea wa nafasi ya urais wa chama hicho, Petter Kuga Mziray alisema chama chake ni tofauti na vyama vingine ambavyo wagombea wanafuatwa na wananchi kwenye viwanja vikubwa, kama vile Jangwani na Kidongo Chekundu, lakini chama chake kinawafuata wananchi kwenye maeneo yao.
Mziray aliahidi kujenga barabara kuu kando kando mwa bahari kutoka Dar es Salaam hadi Tanga katika kipindi chake cha uongozi cha awamu ya kwanza, katika awamu ya pili ya uongozi wake atajenga bara bara kutoka Dar es Salaam hadi Lindi na Mtwara.
Alisema Tanzania ina rasilimali kubwa, lakini chama kilichopo madarakani kimeshindwa kuzitumia na kwamba chama chake kitaimarisha nyanja mbalimbali, ikiwemo kuongeza shule ili wanafunzi wengi waweze kupata nafasi na kujiendeleza kwenye masomo ya elimu ya juu.


Mgombea urais wa chama cha APPT-Maendeleo Petter Kuga Mziray akiwahutubia wananchi katika viwanja vya Buguruni Rozana wakati wa uzinduzi wa kampeni za chama hicho.

MAMA ATOWEKA NYUMBANI MAZINGIRA YA KUTATANISHA


Catherine Cosmas (55), mkazi wa Ubungo Extenal jijini Dar es Salaam,jana ametoweka nyumbani katika mazingira ya kutatanisha juzi saa 3:00 usiku na kwenda kusikojulikana.

Mtoto wa mama huyo Grant Cosmas aliliambia Mwananchi kuwa mama yake aliondoka nyumbani muda huo na kwamba waliagana usiku kwa ajili ya kwenda kulala, lakini alitoka nje na kutokomea moja kwa moja.

Grant alisema kabla ya kuagana walikuwa wakitazama tamthilia na kwamba mama yake anasumbuliwa na ugonjwa wa kusahau baada ya kufanyiwa uperesheni ya kichwa kwa kuwa kichwa kilikuwa kikimuuma mara kwa mara .

Alifafanua kuwa mama yake alikuja Dar es salaam akitokea mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya matibabu tangu Machi mwaka huu na kwamba hawajawahi kupotea tangu afike hapa.

Grant alisema mama huyo alikuwa amevaa nguo ya rangi ya kahawia juu na sketi yenye maua meupe na alikuwa amejitanda khanga rangi nyekungu.

"Tangu amekuja hapa kwa matibabu hakuwahi kupotea, hii ni mara ya kwanza na tumemtafuta tangu jana hatukufanikiwa kumpata,"alisema Grant. Taarifa za kupotea kwa Catherine zimetolewa katika kituo cha polisi cha Urafiki na Muleba cha Mabibo jijini Dar es Salaam.
Alisema endapo mtu yoyote atamuona mama huyo, atoe taarifa katika kituo cha polisi kilichopo Urafiki, Muleba au wapige simu namba 0654 843262, 0717700531 na 0754593244.





Tuesday, August 31, 2010

VYAMA VINNE HAVIJAZINDUA KAMPENI MPAKA SASA

Ndugu wadau, nitaendelea kuwaletea matukio mbalimbali ya uzinduzi rasmi wa kampeni ya vya vingine ambavyo hajazindua mpaka sasa. Vyama ambavyo havijazindua ni TLP, UPDP, NCCR-Mageuzi na APPT- Maendeleo.

Mgombea urais wa TLP ni Mutamwega Mugahywa, UPDP ni Fahmi Dovutwa, NCCR-Mageuzi ni Hashim Rungwe na mgombea urais wa APPT- Maendeleo ni Peter Mziray, lakini Mziray anadai chama chake kimezindua kampeni ingawa hakijaonekana kikifanya hivyo. Baadhi ya wagombea ubunge na udiwani wa vyama hivyo, wameanza kampeni.

Kumekuwepo malalamiko kwa waandishi wa habari kutoandika habari za vyama vingine vidogo. Baadhi ya watu wanadai waandishi wanaandika habari za vyama vitatu tu yaani za Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chadema na za Chama cha Wananchi CUF. Mgombea urais wa APPT- Maendeleo, Mziray anasema waandishi wanaandika habari za vyama ambavyo vinaweza kulipa gharama za waandishi hao. Kwa upande wangu naahidi kufuatilia habari za vyama vingine.

CHADEMA YAZINDUA KAMPENI JANGWANI JIJINI DAR ES SALAAM



Dk Willibrod Slaa akiwatubia wanachama na mashabiki wa Chadema katika uzinduzi wa kampeni za katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam, juzi. Picha zote na Emmanuel Herman.

Wanachama na mashabiki wa Chadema wakimsikiliza mgombea urais wa Chadema, Dk Willibrod Slaa katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kampeni za chama hicho.


Kushoto ni Fred Mpendazoe, katikati John Shibuda na kulia, ni Bob Makani wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni za Chadema kwenye viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam juzi.

USWAZI JIJINI DAR ES SALAAM





Hapa ni Manzese jijini Dar es Salaam

Monday, August 30, 2010

WANAHABARI MMEPOTEA KATIKA TAALUMA YA HABARI

Ndugu mwana mapambano mwenzangu , mwanahabari na mwanaharakati mwenzangu , naomba kutumia fursa hii katika blog yako kuweka wazi au bayana juu ya hoja hii ya taaluma ya habari na vyombo vya habari kukiuka maadili ya kitaaluma .

"Kumeanza pia kujitokeza mtindo wa baadhi ya vyombo vya habari kutoripoti kabisa habari za baadhi ya vyama na wagombea. Baraza linapenda kuwakumbusha wenye vyombo vya habari na wahariri wao kuwa kibali cha kuendesha gazeti au kituo cha radio au runinga ni mali ya umma.

Leseni za vyombo vya habari hutolewa ili umma upewe taarifa; hili ndilo lengo la kwanza. Faida ya kifedha au mapenzi ya kisiasa sio sababu kuu inayofanya leseni ya chombo cha habari itolewe. Kwa hiyo wahariri wajitahidi kufanya kazi yao kwa uadilifu, na wamiliki wa vyombo wasiwashinikize kuacha kutangaza au kuandika habari muhimu katika kipindi hiki."
Hayo si maneno yangu ni manenno ya katibu mtendaji Baraza la Habari Tanzania , aliyosema kwa lengo la kutoa onyo kwa vyombo vya habari na waandishi wa habari .
Naweza kusema kama alijua kuwa wanataaluma ya habari pamoja na vyombo vya habari vimepotea katika taaluma hii , kama ilivyo ada waandishi na vyombo vyake wamekuwa vibaraka wa wagombea wa chama fulani katika kutangaza sera zake , kitendo cha televisheni ya Taifa (TBC) kukatisha hotuba ya mgombea kiti cha urais kupitia chama cha Chadema ni uvunjaji wa sheria na kukiuka haki ya msingi ya wananchi wa Tanzania katika upataji wa taarifa au habari .
Naaamini kabisa katika hali ya kawaida kituo kikubwa kama TBC na kinachoendeshwa kwa kodi za wananchi ni aibu kukatisha matangazo katikati ya hotuba kwa zaidi ya mara moja , ikumbukwe kuwa hii si mara ya kwanza dalili hizi au hali ilishajitokeza hata siku ile ya mgombea wa Chadema alipokuwa anaomba ufadhili .
Ni vyema tukakumbuka kuwa kutokuwepo kwa usawa katika vyombo vya habari ni dalili tosha za kusababisha uvunjaji wa amani ni vyema tukakumbuka juu ya mahuaji ya kimbali kule Rwanda na Burundi sekta ya habari ina nguvu kama sekta zingine za kitaifa , ifahamike kuwa watanzania kwa sasa wanajua haki zao zote na wanafaham nini kinaendele katika Taifa la Tanzania .

Ushauri wangu ni kuwa kwa vile TBC ni chombo cha kitaifa na kinawajibu wa kuwajibika kwa umma ni vyema Mtendaji Mkuu wa hicho chombo awaeleze umma juu ya swala hili kwani kuna hisia kali baina ya TBC na vyama vya upinzani katika kutokuwepo usawa wa kutoa taarifa na mbaya zaidi hii inaonekana wazi .




Mwandishi wa makala haya

ni Samwel Mtuwa

Anapatikana Minnesota ,

United State of America (USA)



Saturday, August 28, 2010

KESI YA KINA JERRY MURO YAAHIRISHWA


Washitakiwa wa kesi ya kuomba rushwa wakijadiliana jambo kwenye kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jana,baada ya kesi yao kuahirishwa mahakamani hapo jana,kutoka kulia ni Edmund Kapama,Deogratias Mgasa na Jerry Muro.Picha na Michael Matemanga
Mtuhumiwa wa kesi ya matumizi mabaya ya fedha kwenye ujenzi wa jengo pacha la Benki Kuu Tanzania (BoT), Amatus Liyumba akiwa kwenye chumba cha Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam,akisubiri kusikiliza rufaa yake mahakamani hapo jana. Picha na Michael Matemanga

Wednesday, August 25, 2010

GARI LA KUBEBA WAGONJWA LIKIWA KWENYE KAMPENI ZA CCM


Gari la kubeba wagonjwa la hospitali ya Rufaa ya Bugando likiwa kwenye msafara wa mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete.

NDOA YA MCHEZA GOLFU MAARUFU DUNIANI YAVUNJIKA SASA


Sasa ni rasmi kwamba mcheza golfu maarufu duniani,Tiger Woods ametalikiana na mke wake, Elin Nordegren baada ya Woods kukiri kwamba alikuwa na mwanamke mwingine. Nordegren and Woods walioana Oktoba 5, mwaka 2004, huko Barbados na wana mtoto wa kike wa miaka mitatu na mwingine wa kiume wa miezi 18. Mpaka sasa haijafahamika Nordegren atapewa shilingi ngapi baada ya kutalikiana, lakini wadadisi wa mambo wanasema Nordegren atapata mamilioni ya dola za Kimarekani.

Tuesday, August 24, 2010

WAGOMBEA WA CUF WAFARIKI ZANZIBAR



Wagombea wawili wa Chama cha Wananchi (CUF) wamefariki dunia jana visiwani Zanzibar katika matukio tofauti.Waliofariki dunia ni alikuwa Mwakilishi wa Jimbo la Kojani (CUF), Omar Ali Jadi (55) Mkoa wa Kaskazini Pemba na Mwalimu Shani Hamada Shani ambaye ni mgombea wa udiwani wa chama hicho katika Jimbo la Kikwajuni. Jadi alikuwa akiugua ugonjwa wa kisukari na kwamba alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya figo. Shani alifariki dunia baada ya kugongwa na gari wakati akielekea kuchukua fomu katika Tume ya Uchaguzi Zanzibar(ZEC), eneo la Maisara.

MAFURIKO PAKISTANI YAENDELEA KUWATESA WATOTO

Mkazi wa Pakistani akiwa amembeba mtoto wake ambaye anaarisha kwenye hospitali ya Sukkur kutokana na athari za mafuriko. Rais wa Pakustani Asif Ali Zardari amesema leo kuwa nchi yake itachukua muda mrefu kuijenga nchi hiyo, kutokana na uharibifu uliosababishwa na marufiko. Dola 700 milioni za Marekani zinahitajika kwa ajili ya kuijenga nchi hiyo. Kutokana na mafuriko hayo, zaidi ya watu 1,500 wamepoteza maisha na wengine milioni 20 wameathirika. Picha na AFP/ Asif Hassan.

Saturday, August 21, 2010

KIKWETE AANGUKA WAKATI AKIHUTUBIA JANGWANI

Kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM), jana zimeingia dosari ikiwa ni siku ya kwanza katika uzinduzi wa kampeni zake katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam baada ya mgombea wake wa kiti cha urais, Jakaya Kikwete kuanguka jukwaani kutokana na kuishiwa nguvu.

Baada ya dakika 16 tangu alipoanza kuhutubia umati wa wanaCCM waliofurika katika viwanja hivyo, Kikwete alianza kuishiwa nguvu na kupepesuka, lakini walinzi wake walimdaka na kumpa msaada kwa kumdoa jukwaani.

Dakika 14 baadaye alirejea jukwaani huku akionyesha kuchoka na kuendelea na hotuba yake kwa dakika tano kabla ya kwenda kuketi meza kuu kwa dakika mbili na kuamua kuondoka katika viwanja hivyo.

Rais Kikwete aliwasili viwanja hivyo saa 7:45 mchana akifuatana na Mgombea Mwenza, Dk Mohamed Gharib Bilal na kupanda katika jukwaa kuu kuungana na viongozi kadhaa wa CCM na serikali akiwa na furaha.

WANACHAMA WA CCM WAKIWA WAMEFURIKA VIWANJA VYA JANGWANI

Friday, August 20, 2010

WATUHUMIWA WA UGAIDI WAKITOKA MAHAKAMANI


Watuhumiwa Hussein Hassan Agad (aliyevaa kanzu nyeusi) na Ismail na Ismail Abubakari wakitoka mahakamani Jumanne iliyopita mjini Kampala nchini Uganda. Watuhumiwa hao, wanadaiwa kuhusika katika mlipuko wa mabomu na kusababisha vifo vya watu 76 nchini humo wakati wakiangalia fainali za kombe la Dunia kati ya timu ya Taifa ya Hispania na Uholanzi. Mechi ya Fainali ilifanyika nchini Afrika Kusini mapema mwaka huu.

WAGOMBEA WA CHADEMA GEITA WAFANYIWA VITUKO


MWENYEKITI wa Chama Cha Maendeleo na Demokrasia (Chasema) Wilaya ya Geita Mabura Kachoji amewashutumu wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa wanawafanyia fujo wagombea udiwani wa chama chao.

Akizungumza na Mwananchi mwenyekiti huyo alibainisha kuwa wafuasi hao wamewafanyiwa fujo wagombea wao wawili na kwamba mgombea udiwani wa kata ya Rwamgasa Jimbo la Busanda Ntalima Masawe Paulo alichomewa Nyumba yake.
Kachoji alidai mbali na kuchomewa nyumba kwa mgombea huyo, Mkuu wa Wilaya ya Geita Philimon Shelutete amekuwa akimkamata Mgombea huyo na kumfuga kwa madai ya kukwamisha shughuli za kimaendeleo.

Alieleza Paulo ametiwa ndani kwa amri ya mkuu huyo wa Wilaya mara tatu na kusababisha ashindwe kufuatilia shughuli za maendelo ya kata yake ambayo anagombea.

“Mimi sidhani kama kuna mtu anaweza kukwamisha shughuli za maendeleo hususani katika eneo ambalo anaishi na wakati huo huo, wananchi wa sehemu hiyo wakiwa wanamunga mkono awe kiongozi wao,”alisema Kachoji.

Alisemja Paulo ni mgombea mwenye sifa ya kuwa kiongozi na anaweza kutetea masilahi ya wananchi na kuleta maendeleo kwa wananchi.

Katika tukio lingine, mgombea wa Kata ya Nyamgusu alivamiwa nyumbani kwake na watu wasiojulikana na kumjeruhi kichwani baada ya kumpiga na nondo.

Kitendo hicho, kimemuathiri mgombea huyo kisaikolojia na amejitoa katika kinyanganyiro na chama kililazimika kumsimamisha mgombea mwingine kupitia Chadema.

Katika hatua nyingine ambayo inaonekana kuwa CCM imedhamiria kuwangoa wapinzani ni kitendo cha baadhi ya maofisa watendaji kufunga ofisi zao mara kwa mara pindi wanapogundua kuwa wagombea wa Chadema wanaenda katika ofisi zao kupata huduma.

Alisema matukio hayo yamekuwa ya kawaida kwa maofisa hao na mtendaji wa Kata ya Katoma alifanya kitendo hicho makusudi cha kutoka nje ya ofisi ili kumkwamisha mgombea wa Chadema wakati alipokuwa akirudisha fomu.

Alisema kutokana na hali hiyo, walifanya kazi ya ziada ya kumtafuta kwa njia ya simu ili waweze kupata huduma, lakini mtendaji huyo aliweka vikwazo vingi kama vile hana usafiri wa kumpeleka ofisini

“Kwa kuwa sisi tulikuwa na shida ilibidi tumfuate na usafiri wa pikipiki tuliokuwa nao,na tulipofika aligoma kupanda pikipiki hiyo kwa madai pikipiki ilikuwa na bendera ya Chadema. Lakini tulipomtishia kuwa tutapeleka malalamiko kwa Mkurugenzi wa Manispaa alikubali kupanda pikipiki,”alisema Kachoji.

Kachoji ilibidi atoe taarifa kwa Mkurugenzi wa Wilaya ya Geita Mpangalakela Katala na mkurugenzi huyo aliahidi kufuatilia malalamiko hayo. Habari hii, imeandikwa na Sheilla Sezzy,Geita

BALOZI WA UHOLANZI AKIZINDUA SHULE YA SEKONDARI LUSHOTO


Balozi wa Uholanzi nchini, Dr Ad Koekkoek akikata utepe wakati wa uzinduzi wa Shule ya Sekondari Prince Claus wilayani Lushoto alipoitembelea juzi. Shule hiyo imepewa jina hilo, ikiwa ni kumbukumbu ya marehemu mume wa Malkia wa Uholanzi, Beatrix Benhard ambaye masomo yake ya awali akiwa mdogo alianzia wilayani. Picha na Burhani Yakub.

FM ACADEMIA KUZINDUA ALBUM MPYA YA VUTA NIKUVUTE

Rais wa Bendi ya FM Academia, Nyoshi El- Saadat (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (pichani hawapo) kuhusu uzinduzi wa album yao ya sita ijulikanayo vuta nikuvute. Uzinduzi huo, utafanyika siku ya Idd Mosi katika Ukumbi wa Diamond Jubilee. Kushoto ni Meneja wa Bendi hiyo, Mujib Khamis na Ofisa Habari wa Idara ya Habari Zahra Majid. Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dar es Salaam

WANANCHI MAMBO SAFIIIIIIIIIIIII, TUTASHINDAAAAA


Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete akiwahutumbia wanachama na wapenzi wa chama hicho kwenye ofisi ndogo za CCM zilizopo Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam jana baada ya kurejesha fomu Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Picha na Edwin Mjwahuzi na Emmanuel Herman.

PROFESA LIPUMBA AKIREJESHA FOMU TUME YA UCHAGUZI



Profesa Ibrahim Lipumba (kushoto) ambaye ni mgombea urais wa CUF na mgombea mwenza, Juma Duni Haji wakisalimia wananchi wakati akiwasili Ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi jijini Dar es Salaam ili kurudisha fomu. Picha na Edwin Mjwahuzi.

Thursday, August 19, 2010

AFUNGWA BAADA YA KUKUTWA AKIUZA ALBINO SH 400 MILIONI


Raia wa Kenya Nathan Mutei (kushoto) jana amefungwa miaka tisa gerezani au kulipa faini ya Sh 80 milioni baada ya kupatikana na hatia ya kusafirisha albino kutoka Kenya kwa lengo la kumuuza Sh 400 milioni. Mtuhumiwa aliondoka Kitale nchini Kenya Agosti 12, mwaka huu na kuingia Tanzania kupitia mpaka wa Isibania kwa ajili ya kumuuza.

Mutei alipofika Tanzania alionana na mganga wa jadi na baadaye taarifa zilitolewa kwa maofisa wa jeshi la polisi kwamba kuna jamaa anauza albino akiwa hai. Kutokana na taarifa hizo, mtuhumiwa alikamatwa na jeshi hilo na baadaye kushtakiwa na kupatikana na hatia.

Mutei alihukumiwa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Mwanza, Angelous Rumisha baada ya kukiri makosa yake katika mahakama hiyo.

Katika kosa la kwanza, Mutei alidaiwa kumsafirisha binadamu kinyume na sheria namba 6 ya mwaka 2008 ya makosa ya kusafirisha binadamu.

Kosa la pili, mtuhumiwa anadaiwa kumteka mtu na kutaka kumuua na kuuza viungo vyake kinyume na kanuni za makosa ya adhabu namba 248 kifungu cha 16. Picha na Frederick Katulanda.

MAFURIKO PAKSTAN YAUA ZAIDI YA WA 1,000 MPAKA SASA

Mafuriko yaliotokea Kaskazini- Magharibi nchini Pakstan, yanakadiriwa kusababisha watu karibu 1,100 kupoteza maisha na wengine milioni moja wameathirika. Kutokana na hali hiyo, wakoaji na Mashirika ya Kimataifa ambayo yanatoa misaada yamekuwa yakiangaika kuokoa maisha ya watu. Umoja wa Mataifa (UN) umesema kuwa watoto wako hatarini kupata magonjwa ya kuambukiza. Marekani imetangaza kutoa msaada wenye thamani ya dola 10 milioni ili kuwasaidia watu walioathirika.  Picha na AFP
Picture by AFP
Picture by AFP

Wednesday, August 18, 2010

MASHABIKI WA YANGA LEO WAKISHANGILIA SIMBA KUFUNGWA MABAO 3-1 KATIKA UWANJA WA TAIFA

KOCHA WA YANGA KOSTADIN PAPIC 'CLINTON' AKIFURAHIA KUIFUNGA SIMBA MAGOLI 3-1

WAFANYAKAZI AFRIKA KUSINI WAANZA MGOMO KUPINGA NYONGEZA YA MSHAHARA

Wafanyakazi nchini Afrika Kusini leo wameanza mgomo rasmi kupinga nyongeza ya asilimia 7 ya mshahara walioongezewa na Serikali nchini humo. Vyama vya wafanyakazi vilivyo chini ya muungano wa Cosatu walipendekeza wafanyakazi waongezewe mshahara kwa asilimia 8.6, lakini serikali imeonekana kutoafiki mapendekezo ya chama hicho.

RAIS KIKWETE AKIZINDUA MNARA WA MASHUJAA WA MAJIMAJI

Rais Jakaya Kikwete akifungua rasmi mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa waliopigana vita vya Majimaji uliojengwa katika Kijiji cha Nandete, Kata ya Kipatimu wilayani Kilwa. Eneo hilo ni mahali ambako vita hivyo vilipangwa na kuanza.Picha na Freddy Maro.

Tuesday, August 17, 2010

MISS TANZANIA WAANZA KAMBI LEO JIJINI DAR ES SALAAM

Warembo wanaowania taji la Miss Tanzania leo watasaini mikataba kati yao na waandaaji pamoja na kupewa semina maalumu na kamati ya mashindano hayo. Mbali na hayo, washiriki 31 kutoka kanda mbalimbali nchini jana walianza kambi kwenye hoteli ya Giraffe nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Monday, August 16, 2010

NDEGE YAKATIKA VIPANDE VITATU, ABIRIA WOTE WATOKA SALAMA


Abiria wote 125 na wafanyakazi sita waliokuwa wamepanda katika ndege Boeing 737 wametoka hai katika ndege hiyo leo baada ya kukatika vipande vitatu wakati ikijaribu kutua katika Kisiwa cha Kolombia. Gavana wa mji wa Bogota amesema ni maajabu watu wote kupona na mtu mmoja tu kufariki dunia katika ajali hiyo.

“Ilikuwa ni maajabu na hatuna budi kumshukuru Mwenyezi Mungu, ni mtu mmoja tu amepoteza maisha,” alisema Ofisa wa Jeshi la Anga nchini Kolombia, Pedro Gallardo (68). Kutokana na ajali hiyo, watu 119 wanatibiwa katika hospitali moja nchini humo na wengine watano ni mahututi katika hospitali hiyo.

KUMEKUCHA MAALIM SEIF ACHUKUA FOMU YA URAIS



Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Khatibu Mwinyichande akimkabidhi fomu za kugombea urais wa Zanzibar, Katibu Mkuu wa Civic United Front (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad (kushoto) kwenye ofisi za tume hiyo,Zanzibar jana. Picha na Emanuel Herman.

Friday, August 13, 2010

MNYIKA ACHUKUA FOMU ZA KUGOMBEA UBUNGE UBUNGO



Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa wa Chadema, John Mnyika (kushoto) leo amechukua fomu za kugombea ubunge katika Jimbo la Ubungo. Amesema katika uchaguzi ujao, amejipanga vizuri na atahakikisha anatafuta kura na kuzilinda ili zisiibwe kama Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005. Picha na Emanuel Herman

CHATU ALIYEPOTEA HUYU HAPA


Wananchi wakiwa wamembeba nyoka aina ya chatu aliyepotea katika eneo la Keko Keko Jijini Dar es Salaam wiki mbili zilizopita na kusababisha hofu kwa wakazi wa eneo hilo, amepatikana jana ndani ya Ofisi za Wizara ya Maliasili na Utalii jijini Da es Salaam.

Mkurugenzi wa Wanyamapori wa Wizara hiyo, Erasmus Tarimo alisema nyoka huyo alipatikana leo saa 4:00 asubuhi ndani ya ofisi hizo baada ya juhudi za timu ya watu wanane kutoka katika kampuni mbalimbali zinazojishughulisha na uwindaji na ufugaji wa viumbe hai pamoja na askari 18 wa wanyamapori.

Baada ya kupatikana kwa nyoka huyo, hivi sasa wakazi wa Keko watalala na kuendelea na shughuli zao za kila siku bila hofu yoyote ya kuumwa na nyoka huyo. Picha na Silvan Kiwale.