Wednesday, September 1, 2010

APPT-MAENDELEO YAZINDUA KAMPENI BUGURUNI


CHAMA cha APPT-Maendeleo kimezindua kampeni yake na kusema kimeweka vipaumbele katika suala la afya, elimu, viwanda na ajira zaidi.
Katika mkutano wa ufunguzi wa kampeni, katika viwanja vya Buguruni Rozana, mgombea wa nafasi ya urais wa chama hicho, Petter Kuga Mziray alisema chama chake ni tofauti na vyama vingine ambavyo wagombea wanafuatwa na wananchi kwenye viwanja vikubwa, kama vile Jangwani na Kidongo Chekundu, lakini chama chake kinawafuata wananchi kwenye maeneo yao.
Mziray aliahidi kujenga barabara kuu kando kando mwa bahari kutoka Dar es Salaam hadi Tanga katika kipindi chake cha uongozi cha awamu ya kwanza, katika awamu ya pili ya uongozi wake atajenga bara bara kutoka Dar es Salaam hadi Lindi na Mtwara.
Alisema Tanzania ina rasilimali kubwa, lakini chama kilichopo madarakani kimeshindwa kuzitumia na kwamba chama chake kitaimarisha nyanja mbalimbali, ikiwemo kuongeza shule ili wanafunzi wengi waweze kupata nafasi na kujiendeleza kwenye masomo ya elimu ya juu.

No comments:

Post a Comment