Wacheza ngoma ya asili wakionyesha staili mbalimbali za kucheza kwenye sherehe ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa, William Lukuvi kufungua jengo jipya la uzazi na upasuaji katika Zahanati ya Roundtable iliyopo Mbagala jijini Dar es Salaam.
Friday, August 13, 2010
LUKUVI KATIKA MOJA YA KAZI ZAKE DAR ES SALAAM
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi akitoa pongezi kwa watengenezaji wa meza ya maabara yakuhamishika pamoja na kuizindua Shule ya Sekondari ya Mbagala Kuu jijini Da es Salaam. Meza hiyo, ina thamani ya shilingi 5 milioni na imenunuliwa na Manispaa ya Temeke ili kuwasaidia wanafunzi shuleni hapo kufanya mazoezi ya vitendo.
Thursday, August 12, 2010
NAPE HUYOOO AIBUKIA CHADEMA
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Nape Nauye jana alienda kwenye Mkutano Mkuu wa Chadema na bila kuchelewa wajumbe wa mkutano huo, walikuwa wakijaribu kumvika tagi yenye picha ya mgombea wa urais wa Chadema, Dk Willibrod Slaa. Awali ilielezwa kuwa Nape alikuwa anataka kujiunga na Chadema baada ya kuangushwa kwenye kura za maoni katika Jimbo la Ubungo jijini Dar es Salaam. Lakini jana Nape alisema ni mwanachama wa CCM na ataendelea kubaki CCM.
SAMUEL SITTA NA ROSTAM AZIZI WAKITETA JAMBO
Viongozi hawa; Spika wa Bunge, Samuel Sitta akiteta na Mbunge wa Igunga, Rostam Azizi kwenye Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi mjini Dodoma jana.
WAZIRI WA ZAMANI AFIKISHWA MAHAKAMANI
Waziri wa mkongwe wa serikali ya awamu ya kwanza hadi ya nne na aliyekuwa Mbunge wa Mufindi Kaskazini, Joseph Mungai amefikishwa jana katika Mahakama ya Mkoa wa Iringa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa tuhuma za kutoa rushwa wakati wa kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Kesi yake iko kwa Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Iringa, Mary Senape na kwamba anatuhumiwa kufanya kosa hilo Julai 8, mwaka huu katika Kata ya Ihalimba.
AKATWA KWA PANGA KWA KUTOJUA KUPIKA CHAKULA KITAMU
Mkazi wa Kijiji cha Itununu wilayani Serengeti, Juliana Mark (20) akiwa amelazwa katika hospitali ya wilaya hiyo baada kukatwa na panga kichwani, mkononi na mguuni kwa kuwa hajui kupika chakula kizuri.
WANACHAMA CCM WACHARUKA KURA ZA MAONI
Wanachama wa CCM jijini Dar es Salaam wakilalamika kwa Katibu Uenezi na Siasa Mkoa wa Dar es Salaam wa chama hicho, Juma Simba kuwa wagombea wao waliotangazwa washindi katika kura za maoni wameenguliwa.
Picha zote na Michael Jamson, Tumaini Msowoya, Anthony Mayunga na Edwin Mjwahuzi.
HII NDIO BONGO DAR ES SALAAM
Wafanyabiashara ndogondogo (wamachinga) wakiwa wamepanga bidhaa chini katika barabara ya Uhuru sehemu ya waenda kwa miguu eneo la Karume jijini Dar es Salaam.
Friday, August 6, 2010
MKE WA OBAMA 'AKITANUA' HISPANIA
Mke wa rais wa Marekani, Michelle Obama (mwenye miwani) akiwa nchini Hispania jana kwa ajili ya kutembelea mji wa kihistoria wa Marbella. Katika ziara hiyo, Michelle ameongozana na mtoto wake Sasha, wanaoonekana pembeni yake walinzi na mafariki wa familia ya rais Obama. Jamaii imekuwa ikilalamikia zaidi gharama anazotumia Michelle katika ziara zake za mapumziko.
WANAFUNZI 18 WAFA MAJI ZIWANI
KATIKA Mkoa wa Mwanza wanafunzi 18 wa Shule ya Msingi ya Chekechea ya Halukunbi wamefariki dunia baada ya mtumbwi waliokuwa wakisafiria kuzama kwenye Ziwa Victoria.
Kamanda wa polisi mkoani Mwanza,Simon Sirro alisema ajali hiyo, ilitokea jana saa 1:45 asubuhi wakati wanafunzi wanaokadiriwa kuwa 37 walipokuwa wakisafiri kutoka Kisiwa cha Chitambele kwa ajili ya kwenda Kijiji cha Hulukumbi katika Wilaya ya Sengerema.
Kamanda wa polisi mkoani Mwanza,Simon Sirro alisema ajali hiyo, ilitokea jana saa 1:45 asubuhi wakati wanafunzi wanaokadiriwa kuwa 37 walipokuwa wakisafiri kutoka Kisiwa cha Chitambele kwa ajili ya kwenda Kijiji cha Hulukumbi katika Wilaya ya Sengerema.
DK SLAA: WAFANYAKAZI NCHINI NIPIGIENI KURA ZENU 350,000
CHAMA cha Maendeleo na Demokrasia (Chadema), kinaonekana kuwa na ushawishi mkubwa kwa wananchi na sasa kimewataka Watanzania, wakiwemo wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wafanyakazi 350,000 kumpigia kura mgombea urais wa Chadema katika uchaguzi mkuu ujao.
Mapema mwaka huu, Rais Jakaya Kikwete akizungumza na wazee wa Dar es Salaam baada ya Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA)kutangaza mgomo nchi mzima kuanzia Mei 15, mwaka huu, alisema hataki kura 350,000 za wafanyakazi hao, kwani ana uhakika wa kushinda nafasi ya urais oktoba. Kwa mujibu wa Dk Willibrod Slaa, Rais Kikwete alisema hata kama wafanyakazi wote wasipomchagua hana haja na kura zao.
Hayo yalisemwa mkoani Mtwara katika mkutano wa hadhara jana uliofanyika viwanja vya mashujaa mjini hapa wakati Dk Slaa akiomba kudhaminiwa na wananchi ili kugombea nafasi ya urais.
Thursday, August 5, 2010
FAHARI YA TANZANIA
Hii ni fahari ya Tanzania. Watanzania tujivunie maliasili zetu. Kiboko akiwa katika hifadhi ya SERENGETI.
Wednesday, August 4, 2010
WAFUASI WA DK SLAA NA WA RAIS KIKWETE WAZOMEANA
WAFUASI wa mgombea urais kwa chama cha Chadema Dk Willibrod Slaa na wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliokuwa wakisubiri kumdhamini Rais Jakaya Kikwete nusura wazue mtafaruku baada kupishana na kuzomeana.
Tukio hilo lilitokea saa 6:30 mchana wakati wafuasi wa Chadema walipokuwa wametoka kumpokea Dk Slaa uwanja wa ndege wakapishana katika eneo la ofisi za CCM mkoa walipokuwapo wale wa CCM wakisubiri kumdhamini Rais Kikwete katika harakati zake za urais.
MREMA ASHANGILIA KIMARO KUANGUSHWA VUNJO
MWENYEKITI wa Tanzania Labour Party (TLP), Agustino Mrema, jana alitembea zaidi ya kilometa 10 kwa miguu kuudhihirishia umma kuwa ana afya nzuri wakati akienda kuchukua fomu za kugombea Ubunge katika Jimbo la Vunjo.
Mrema akiwa na mgombea urais kupitia tiketi ya chama hicho,Mutamwega Mganywa, walitembea kwa miguu kutokea Kijiji cha Chekereni hadi mji mdogo wa Himo,huku akisindikizwa na mamia ya wanachama.
Wanachama hao wakiwa wamevalia fulana za njano zenye nembo ya TLP na maneno "Vunjo hatudanganyiki", walikuwa wakishangilia na vijana waliokuwa wakiendesha pikipiki zaidi ya 40, wakifanya vituko mbalimbali kama ishara ya kushangilia.
Mrema aliwapongeza wanachama wa CCM wa Jimbo la Vunjo kwa kuamuangusha Mbunge aliyemaliza muda wake, Aloyce Kimaro katika kura za maoni.
"Wana-CCM Vunjo ni watu wazuri sana hongereni kwani mlichokifanya ni jambo zuri la kumuondoa Kimaro. Kimaro ana fedha nyingi hivyo, angenisumbua sana,"alitamba Mrema.
Katika mchakato wa kura za maoni, Wakili na Mwanasheria wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii(NSSF), Chrispin Meela aliongoza kwa kupata kura 7,732 dhidi ya Kimaro aliyepata kura 3,207 na hivyo kushindwa kutetea kiti chake.
UMATI WA WANAFUNZI WAKIFANYA MTIHANI ILI WAAJIRIWE
WANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakifanya mtihani jana katika chuo hicho, ulioandaliwa na kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) kwa ajili ya kuwaajiri katika kampuni hiyo. Umati wa wanafunzi hao, unaonyesha jinsi tatizo la ajira lilivyokubwa nchini. Pengine wanaohitajika kuajiriwa ni watu sita tu kati ya watu 200 waliofanya mtihani.
WANAFUNZI 80 WANUSURIKA KUTEKETEA KWA MOTO
WANAFUNZI 80 waliokuwa wamelala katika bweni la Nyerere Shule ya Sekondari Rugambwa Manispaa ya Bukoba wamenusurika kufariki dunia baada ya bweni hilo kuteketea kwa moto usiku wa kuamkia jana. Tukio hilo, lilitokea saa 2:30 usiku wakati wanafunzi hao wakiwa wanasoma madarasani.Katika tukio hilo, vifaa vyote vya wanafunzi viliteteketea kwa moto.
Mwandishi wa Mwananchi ambaye alikuwa eneo la tukio alishuhudia zaidi ya wanafunzi 15 wakizimia na kupoteza fahamu na baadaye kukimbizwa katika hospitali ya mkoa Kagera kwa matibabu zaidi. Mazingira ya shule hiyo yalitawaliwa na vilio vya wananchi na wanafunzi katika giza nene na kamanda wa polisi wa Mkoa wa Kagera Henry Salewi alikuwa miongoni mwa viongozi walioshiriki kuimarisha usalama katika eneo hilo.
Mkuu wa sekondari hiyo ya wasichana Asha Mbanga alipoulizwa kwa njia ya simu alisema hana taarifa kuhusu tukio hilo kwani alikuwa safarini kutoka jijini Mwanza.
Mwandishi wa Mwananchi ambaye alikuwa eneo la tukio alishuhudia zaidi ya wanafunzi 15 wakizimia na kupoteza fahamu na baadaye kukimbizwa katika hospitali ya mkoa Kagera kwa matibabu zaidi. Mazingira ya shule hiyo yalitawaliwa na vilio vya wananchi na wanafunzi katika giza nene na kamanda wa polisi wa Mkoa wa Kagera Henry Salewi alikuwa miongoni mwa viongozi walioshiriki kuimarisha usalama katika eneo hilo.
Mkuu wa sekondari hiyo ya wasichana Asha Mbanga alipoulizwa kwa njia ya simu alisema hana taarifa kuhusu tukio hilo kwani alikuwa safarini kutoka jijini Mwanza.
ALAWITIWA BAADA YA KUNYWA POMBE NYINGI
JESHI la polisi linamshikilia mkazi mmoja wa Kijiji cha Kalungwa Tarafa ya Mkuyuni Wilaya ya Morogoro kwa tuhuma za kumlawiti mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 31.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Thobias Andengenye alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea Agosti 1 mwaka huu,saa 2:30 katika kijiji hicho baada ya mtu huyo kupoteza fahamu baada ya kunywa pombe kupita kiasi na kulewa chakari.
Alimtaja mtuhumiwa wa tukio hilo kuwa ni Bahati Said na kwamba mtu huyo alilawitiwa wakati akitokea kilabuni baada ya kuzidiwa na pombe na kusababisha kuanguka na kulala vichakani na mtuhumiwa huyo wakati akipita katika eneo hilo, alimkuta na kumlawiti. Mtu huyo ametibiwa katika hospitali ya Mkoa wa Morogoro na kwamba uchunguzi zaidi wa polisi unaendelea kuhusiana na tukio hilo .
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Thobias Andengenye alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea Agosti 1 mwaka huu,saa 2:30 katika kijiji hicho baada ya mtu huyo kupoteza fahamu baada ya kunywa pombe kupita kiasi na kulewa chakari.
Alimtaja mtuhumiwa wa tukio hilo kuwa ni Bahati Said na kwamba mtu huyo alilawitiwa wakati akitokea kilabuni baada ya kuzidiwa na pombe na kusababisha kuanguka na kulala vichakani na mtuhumiwa huyo wakati akipita katika eneo hilo, alimkuta na kumlawiti. Mtu huyo ametibiwa katika hospitali ya Mkoa wa Morogoro na kwamba uchunguzi zaidi wa polisi unaendelea kuhusiana na tukio hilo .
Mtikila akwepa kifungo gerezani
MWENYEKITI wa DP, Mchungaji Christopher Mtikila amekubali kulipa deni alilokuwa anadaiwa na Paskazia Matete la Sh 9.8 milioni na kuachiwa huru.
Kama Mchungaji huyo ambaye ametangaza kugombea urais kupitia chama chama cha DP asingelipa deni hilo, angetumikia kifungu cha miezi sita gerezani na tayari juzi alianza kuonja joto la jiwe baada ya kulala mahabusu ya kituo cha polisi cha Msimbazi kwa kushindwa kulipa deni hilo.
Mtikila alihukumiwa kifungo cha miezi sita jela bila ya kuwepo mahakamani Julai 29 baada ya mahakama kukubali ombi la mdai huyo. Hakimu Joyce Minde alitoa hukumu hiyo kwa sharti kwamba ianze kutekelezwa baada ya Paskazia kulipa Sh600,000 kwa ajili ya gharama za kumhudumia mchungaji huyo wakati atakapokuwa kifungoni.Mwanamke huyo alilipa fedha hizo na ndipo hukumu hiyo ilipoanza kutekelezwa.
Tuesday, August 3, 2010
Utata wa Malecela na Lusinde watatuliwa
Hatimaye CCM wilayani Chamwino jana ilimaliza utata kwenye matokeo ya kura za maoni katika jimbo la Mtera ilipotangaza kuwa mwanasiasa mkongwe, John Malecela ameangushwa baada ya habari kusambaa kwa kasi kubwa kuwa Livinstone Lusinde hakuwa ameshinda.
Habari za ushindi wa Lusinde zilifunikwa na taarifa iliyosambaa kwa kasi jana kuwa mshindi wa kura za maoni kwenye jimbo hilo bado hajatangazwa rasmi na kwamba Malecela ndiye aliyekuwa akiongoza kwa kupata kura 5,652 dhidi ya 5,407 za Lusinde licha ya katibu wa CCM mkoani Dodoma kumtangaza kijana huyo kuwa ndiye mshindi.
Lakini jana, mkurugenzi wa uchaguzi wa CCM wilayani Chamwino ambaye pia ni katibu wa chama hicho kwenye wilaya hiyo, Edson Lihweuli aliitisha mkutano na waandishi wa habari na kumtangaza Lusinde kuwa mgombea wa ubunge kwa tiketi ya CCM kwenye uchaguzi mkuu ujao na hivyo kuthibitisha habari za kuanguka kwa Malecela, maarufu kama "tingatinga".
Subscribe to:
Posts (Atom)







