Mrembo wa Vodacom Miss Tanzania 2010, Genevieve Emmanuel akiwa kwenye gari aina ya Hyundai baada ya kushinda taji la urembo usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Gari hilo, alikabidhiwa na Mkurungezi Mtendaji wa Vodacom Dietlof Mare. (Picha zote na Venance Nestory)
Sunday, September 12, 2010
Baadhi ya wageni wakifuatilia shindano la kumtafuta Miss Tanzania, lililofanyika usiku wa kuamikia leo katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Tuesday, September 7, 2010
WAREMBO WAKIWA WAMEPOZI KATIKA SHINDANO LA KUMTAFUTA BALOZI WA REDDS
Washiriki 30 wakiwa wamepozi katika shindano la kumsaka Balozi wa Redds lililofanyika Kinyamwezi Pub, Mikocheni. Mshindi wa atatangazwa Jumamosi katika shindano la kumtafuta Miss Tanzania.
TENDWA AIONYA CCM
John Tendwa ambaye ni msajili wa Vyama Vya Siasa nchini amekishauri Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutotumia picha zilizopigwa katika maeneo ya Ikulu kwenye kampeni zake kwa kuwa zinawashawishi wananchi kukipigia kura na kwamba vyama vingine vya siasa haviwezi kuzipata picha hizo kutokana na kutoweza kupiga picha kwenye eneo la Ikulu.
Wednesday, September 1, 2010
OBAMA AWAZUIA WATOTO WAKE KUTAZAMA TELEVISHENI
Rais wa Marekani Barack na mke wake, Michelle Obama wakiwa wameongozana na watoto wao, Malia Obama (12) na Sasha (9) ambaye baba yake amemshika begani. Wazazi hao, wamesema wanataka watoto wao waishi maisha ya kawaida na pia hawaruhusiwi kutazama televisheni katikati ya wiki na kompyuta wamekuwa wakitumia kwa ajili ya kufanya kazi za shule tu. Obama na Michelle hakuwakueleza ni kwanini wanawazuia watoto hao kuangalia televisheni muda mrefu.
APPT-MAENDELEO YAZINDUA KAMPENI BUGURUNI
CHAMA cha APPT-Maendeleo kimezindua kampeni yake na kusema kimeweka vipaumbele katika suala la afya, elimu, viwanda na ajira zaidi.
Katika mkutano wa ufunguzi wa kampeni, katika viwanja vya Buguruni Rozana, mgombea wa nafasi ya urais wa chama hicho, Petter Kuga Mziray alisema chama chake ni tofauti na vyama vingine ambavyo wagombea wanafuatwa na wananchi kwenye viwanja vikubwa, kama vile Jangwani na Kidongo Chekundu, lakini chama chake kinawafuata wananchi kwenye maeneo yao.
Mziray aliahidi kujenga barabara kuu kando kando mwa bahari kutoka Dar es Salaam hadi Tanga katika kipindi chake cha uongozi cha awamu ya kwanza, katika awamu ya pili ya uongozi wake atajenga bara bara kutoka Dar es Salaam hadi Lindi na Mtwara.
Alisema Tanzania ina rasilimali kubwa, lakini chama kilichopo madarakani kimeshindwa kuzitumia na kwamba chama chake kitaimarisha nyanja mbalimbali, ikiwemo kuongeza shule ili wanafunzi wengi waweze kupata nafasi na kujiendeleza kwenye masomo ya elimu ya juu.
Mgombea urais wa chama cha APPT-Maendeleo Petter Kuga Mziray akiwahutubia wananchi katika viwanja vya Buguruni Rozana wakati wa uzinduzi wa kampeni za chama hicho.
MAMA ATOWEKA NYUMBANI MAZINGIRA YA KUTATANISHA
Catherine Cosmas (55), mkazi wa Ubungo Extenal jijini Dar es Salaam,jana ametoweka nyumbani katika mazingira ya kutatanisha juzi saa 3:00 usiku na kwenda kusikojulikana.
Mtoto wa mama huyo Grant Cosmas aliliambia Mwananchi kuwa mama yake aliondoka nyumbani muda huo na kwamba waliagana usiku kwa ajili ya kwenda kulala, lakini alitoka nje na kutokomea moja kwa moja.
Grant alisema kabla ya kuagana walikuwa wakitazama tamthilia na kwamba mama yake anasumbuliwa na ugonjwa wa kusahau baada ya kufanyiwa uperesheni ya kichwa kwa kuwa kichwa kilikuwa kikimuuma mara kwa mara .
Alifafanua kuwa mama yake alikuja Dar es salaam akitokea mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya matibabu tangu Machi mwaka huu na kwamba hawajawahi kupotea tangu afike hapa.
Grant alisema mama huyo alikuwa amevaa nguo ya rangi ya kahawia juu na sketi yenye maua meupe na alikuwa amejitanda khanga rangi nyekungu.
"Tangu amekuja hapa kwa matibabu hakuwahi kupotea, hii ni mara ya kwanza na tumemtafuta tangu jana hatukufanikiwa kumpata,"alisema Grant. Taarifa za kupotea kwa Catherine zimetolewa katika kituo cha polisi cha Urafiki na Muleba cha Mabibo jijini Dar es Salaam.
Alisema endapo mtu yoyote atamuona mama huyo, atoe taarifa katika kituo cha polisi kilichopo Urafiki, Muleba au wapige simu namba 0654 843262, 0717700531 na 0754593244.
Subscribe to:
Posts (Atom)